Ijumaa , 6th Nov , 2015

Chama cha mpira wa kikapu mkoa wa Dar es salaam BD kinatarajiwa kupeleka timu mbili katika michuano ya kombe la taifa litakaloanza Novemba 22-28 mwaka huu Mkoani Dodoma.

Rais wa BD Mwenze Kabinda amesema, wameanza maandalizi ya kuandaa timu hizo zitakazokwenda kuwakilisha mkoa wao.

Kabinda amesema, timu zitakazokwenda kushiriki kombe hilo ni mabingwa watetezi kutoka wilaya ya Temeke na nyingine itakayoundwa na wachezaji kutoka Ilala na Kinondoni.

Kabinda amesema, mwaka jana mkoa wa Dar es salaam uliwakilishwa na timu moja kutoka wilaya ya kinondoni ambao walikuwa mabingwa watetezi.

Kabinda amesema kutokana na wingi wa wachezaji wanaocheza mpira wa kikapu wameamua kuongeza timu nyingine ili kwenda kushiriki michuano hiyo.