
Katibu mkuu wa chama cha mpira wa wavu mkoa wa Dar es salaam DAREVA Yusuph Mkalambati amesema, timu hizo zitapatikana Desemba 29 mwaka huu baada ya kumalizika kwa mashindano ya wavu ufukweni.
Mkalambati amesema, timu nne ambazo zitafanya vizuri katika mashindano hayo zitauwakilisha mkoa wa Dar es salaam katika masshindano ya kombe la Taifa.
Mkalambati amesema, mashindano ya ufukweni yanaendelea yanashirikisha timu za klabu za mkoa wa Dar es salaam yakiwa na lengo la kuweza kupata wachezaji azuri watakaoendeleza kutangza mchezo huo ndani na nje ya nchi.