Jumatano , 21st Oct , 2015

Serikali ya Tanzania imetoa taarifa kwa shirika la afya duniani (WHO) kuhusu kuongezeka kwa ugonjwa kipindupindu nchini huku aina mpya ya kirusi kungundulika jijini Dar-es-Salaam tarehe 25 Agosti.

WHO inasema, ripoti ya hivi karibuni inaonesha kipindupindu kimesambaa katika mikoa 13 nchini Tanzania na sasa kimefika kisiwani Zanzibar.

Christian Lindenmeyer ni msemaji wa WHO amesema wagonjwa 4,324 wa kipindupindu wameriptiwa ikiwemo vifo 67 ambapo ugonjwa huo umeingia visiwani Zanzibar ambako wagonjwa 106 wameripotiwa.

WHO inasema, kipindupindu kimeathiri pia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ambapo visa zaidi ya elfu tatu vimeripotiwa pamoja na vifo 91.

Wakati huohuo huo watu kumi na saba wamepoteza maisha na wengine miasaba themanini na tano wamelazwa katika vituo vinne kutokana na ugonjwa wa kipindupindu katika halmashauri ya wilaya ya Singida kwa kipindi cha kuanzia Septemba hadi Oktoba mwaka huu.

Kaimu mganga wa halmashauri ya wilaya ya Singida Dkt. Paul Maiga amesema hayo wakati walipokuwa wakipokea vibuyu chirizi elfu nne mia sita kutoka shirika lisilo la kiserikali la World Vision Tanzania kwa ajili ya kunawia mikono pindi wananchi wanapotoka chooni kwa lengo la kupunguza maambukizi .