Alhamisi , 1st Oct , 2015

Lile sakata la kufungiwa kwa wimbo wa msanii wa Bongo Flava Roma mkatoliki wa ViVa Roma, bado linaendelea kuwa hewani baada ya Roma leo kusema kwamba anaiamini BASATA na hawawezi kuufungia wimbo wake.

Roma amfunguka hayo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, na kusema kwamba anaamini BASATA wanamsapoti na zilizopo ni fununu tu kwa kuwa hakuna barua rasmi iliyoletwa kwake.

"BASATA wanasapoti kazi za wasanii, kwa hiyo huwezi kuniambia kwamba wimbo wa Roma umefungiwa, BASATA hawawezi kutoa maamuzi kama hayo ya kufungua ngoma ya Roma, me i'm sure BASATA wanasapoti kazi ya sanaa na wanamsapoti Roma, na hizi taarifa nazichukulia tu kama rumors", alisema Roma.

Roma aliendelea kwa kusema kwamba mpaka leo hakuna barua rasmi aliyopewa, kuhusu kufungiwa kwa wimbo huo.

"Kwanza hakuna Officia leter ambayo nimepewa, pili nikiangalia mifano kama ambayo nimekupa na vyenye ambavyo wao wamesema kwa mtazamo wao, hapana kwa chombo kama BASATA hawawezi kuangalia kwa jicho hilo, ni nawaamini BASATA na najua kabisa lazima wasapoti kazi zangu", alisema Roma.