
Msanii wa maigizo, muimbaji, Mtunzi na Mchekeshaji Patcho Mwamba
Star huyo amejipanga kwa ajili ya kutengeneza kipindi kitakachosimama kwa jina la Bana Congo ambacho atawafahamisha mashabiki zaidi juu yake mara baada ya uchaguzi.
Patcho ameiambia eNewz kuwa kwa sasa hana filamu yoyote kubwa ambayo anatayarisha kama yeye, isipokuwa amekuwa akishiriki katika filamu za watu hapa na pale, kuonesha kuwa hajaweka uigizaji pembeni, akiendelea kujijengea sifa kubwa ya kuwa kati ya wasanii wachache wenye uwezo wa kufanya mambo mbalimbali kwa kiwango cha juu kwa wakati mmoja.
