Meneja Mawasiliano wa Tanesco Adrian Mvungi
Ufafanuzi huo umetolewa leo jijini Dar es salaam na Meneja wa mawasiliano wa TANESCO Adrian Mvungi wakati wakikabidhi madarasa ya shule ya Msasani B yaliyotandazwa nyaya za umeme na shirika hilo kwa lengo la kusaidia shule hiyo kufundishia kwa mbinu za kisasa kwa kutumia kompyuta.
Mvungi amesema kuwa kwasasa wanawasha mitambo ya gesi kwa zamu ndio maana zoezi limechukuwa muda mrefu.
Kwa Upande wa mkuu wa shule ya Msasani B Mario Gandi amesema nishati ya umeme itasaidia walimu katika kazi zao pamoja wanafunzi kujisomea wakati wa usiku.
Gandi ameongeza kuwa bado kuna changamoto nyingine kama uchakavu wa sakafu madarasi pamoja na mapaa, ukuta kwa ajili ya ulinzi.



