Alhamisi , 17th Sep , 2015

Msanii wa muziki Pam Daffa, akiwa katika kundi la wasanii ambao misimamo yao kisiasa ni suala ambalo wameamua kuliweka binafsi, amesema kuwa hatua hiyo imezuia yeye na wasanii wenye msimamo kama wake kukosa mashavu ya kutumbuiza.

Msanii wa muziki wa bongofleva Pam Daffa

Ikiwa inafahamika vyema kuwa majukwaa ya kisiasa ni nafasi nzuri kwa wasanii kutengeneza pesa, Pam Daffa amesema kuwa, kidemokrasia ana haki ya kutoonyesha msimamo, ingawa pia ana utayari wa kupanda katika jukwaa la chama chochote kwa kufanya kazi ya kutumbuiza tu.