Jumatano , 2nd Sep , 2015

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ameviaga vikosi vya usalama nchini huku akijivunia ufanyaji wao kazi na kuiweka nchi salama pamoja na raia wake licha ya changamto wanazokumbana nazo.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride rasmi liliandaliwa na vikosi mbalimbali wakati wa sherehe ya kuagwa rasmi na vyombo vya Usalama.

Akiongea jana katika Hafla ya kuyaaga majeshi hayo likiwemo jeshi la Wananchi, JWTZ, Jeshi la Kujenga Taifa, Jeshi la Polisi na Magereza rais kikwete amesema serikali bado ipo katika mchakato wa kuboresha mazingira ya Walinzi hao wa nchi na raia wake yawe bora zaidi.

Dkt. Kikwete ameongeza kuwa katika kipindi chake moja kati ya mafanikio aliyoyafanya ni pamoja na kujenga umoja baina ya vikosi hivyo vya usalama ikiwemo katika ushirikiano wa Ulinzi wa nchi pamoja na raia wake.

Rais Kikwete ameongeza kuwa Serikali ipo katika Ujenzi wa nyumba elfu kumi za Jeshi la Wananchi lakini pia wako katika mchakato wa kuomba msaada kutoka china kwa ajili ya kujenga nyumba zingine elfu kumi za jeshi la polisi nchini Tanzani kazi ambayo ameahidi ataicha kwa amiri Jeshi Mkuu atakefata.

Aidha Dkt. Kikwete amewataka vikosi hivyo vya usalama kutoa ushirikiano kama waliompatia yeye katika kulinda amani ya nchi kwa kiongozi yoyote atakayefuata kuliongoza taifa baada ya uchaguzi mkuu ujao.

Katika hafla hiyo ambayo ilipambwa na bendi mbalimbali za utumbuizaji za jeshi ambapo kuna kipindi ilionekana uzalendo kumshinda Rais Kikwete na kuanza kuimba wimbo uliokuwa unapigwa na bendi moja wapo.