
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Nchini TFF, Celestine Mwesigwa amesema vilabu vyote vilishakamilisha usajili tangu kufungwa kwa usajili wa mara ya kwanza Agost 20 isipokuwa vilabu vya Coastal Union ya Tanga, Toto Africa ya Mwanza na Stand United ya Shinyanga ambapo mpaka sasa navyo vimekamilisha usajili huo kwa kukamilisha kila kinachotakiwa kwa wachezaji wa ndani.
Mwesigwa amesema, kwa upande wa wachezaji wa kimataifa hati zao za uhamisho ITC zitatakiwa kukamilika Agost sita na iwapo ITC zao zitakuwa hazijafika mpaka muda huo hawataruhusiwa kutumia wachezaji wao japo watakuwa wameshawasajili.
Dirisha la usajili lilifunguliwa Juni 15 ambapo lilitarajiwa kufungwa Agost sita lakini TFF ilipeleka mbele usajili huo mpaka Agost 20 kwa kuvipa vilabu vyote nafasi ya kuweza kukamilisha usajili huo ambapo mpaka Agost 20 vilabu vitatu vilikuwa havijakamilisha lakini vilabu vyote vilipewa nafasi ya kuendelea na usajili mpaka Agost 31 lakini kwa faini ya shilingi laki tano kwa kila mchezaji.