usahili wa kwanza Dance100%2015 uliofanyika TMK jijini Dar es Salaam
Kundi la Team Shamba , The WT Group, WD, The Best Boys kaka Zao na Team Makorokocho wameweza kushinda nafasi ya kuingia katika michuano kutoka wilaya ya Temeke.
Makundi haya yamechuana vikali na mengine 7 yanayokamilisha idadi ya makundi 11 ambayo ni jumla ya makundi yote yaliyofika ambayo ni UNI 6 Crew, GMF Crewm TWC, Dar Crew, Noma Sana Crew, Viga Stars yaliyojitokeza kuwania nafasi hiyo katika usaili huo wa kwanza.
Majaji Super Nyamwela, Queen Darlen na Shetta wametumia umakini mkubwa kuhakikisha wanatoa alama zinazostahili kwa mujibu wa vigezo kutoka washiriki wote, huku burudani mbalimbali zikijiri na kushereheshwa kikamilifu na watangazaji rasmi wa Dance 100% kwa mwaka huu akiwemo Tbway 360 na Maggie Vampire.