Alhamisi , 23rd Jul , 2015

Msanii wa muziki Akothee kutoka nchini Kenya, amefungua moyo wake na kusaidia kugharamia ada za watoto wawili kutoka mazingira magumu, kuwawezesha kujiendeleza kielimu ikiwa ni hatua pia ya kukumbusha mashabiki wake kujali yatima na ndugu zao.

Msanii wa muziki Akothee kutoka nchini Kenya akiwa na vijana aliojitolea kuwasaidia

Msanii huyu ambaye amekuwa muwazi kuanika mafanikio na harakati zake, hasa akijivunia mazingira magumu na ya umasikini, amezigusa hisia za wengi kwa hatua yake hii, hasa ikizingatiwa kuwa binafsi tayari ana familia kubwa ambayo inamtegemea.

Akothee anabaki katika kumbukumbu za wengi kupitia kisa chake cha kuachika akiwa na umri mdogo tu wa miaka 14, bila chochote akiwa na jukumu la kulea watoto wanne peke yake katika kipindi hicho.