Jumatatu , 29th Jun , 2015

Katika kuelekea kuanza kwa safari ya kuwasaka wakali wa kudansi nchini Tanzania kupitia mashindano makubwa ya Dance 100% 2015, wito umetolewa kwa wale wote wenye vipaji vya kusakata dansi mitaani kuanza kujipanga na kujinoa kwa usahili.

mashindano makubwa ya Dance 100% 2015 nchini Tanzania

Kama ambavyo utaratibu ulivyotangazwa kwa wanaonuia kushiriki Dance100%, 2015 tayari kwa usahili wa michuano hiyo itakayoanza hivi karibuni, wanatakiwa kuunda makundi ya watu 5 hadi 8, na kuanza mazoezi tayari kabisa kwa kuleta ushindani wa nguvu pale usahili utakapoanza.

Baada ya kung'ara kwa makundi makali kabisa kupitia Dance 100 miaka iliyopita, wakiwemo T AFRICA, THE CHOCOLATE na WAKALI SISI sasa ni Zamu Yako, kaa tayari kwa Dance100% 2015.