Jumatano , 24th Jun , 2015

Msanii bora anayechipukia wa mwaka huu, Barakah Da Prince ameweka wazi kuwa anajivunia kuweza kufikia mafanikio makubwa ndani ya kipindi cha mwaka mmoja pekee, kutoka kwenye U-underground na kuweza kutikisa chati mbalimbali za kimataifa.

Barakah Da' Prince

Barakah, tofauti na wasanii wengine ambao huanza kufanya vizuri ndani ya mipaka ya nchi pekee, amesema nafasi hiyo imekuwa ni ya kipekee kwake hasa ikizingatiwa kuwa kwa sasa yeye ni moja kati ya mastaa wanaoipeperusha vyema bendera ya Tanzania nje ya mipaka yake.

Star huyo pia ametaka mashabiki wake kufahamu mpango wake wa kuendeleza moto huo, akiwa anajitayarisha kwaajili ya kuachia rekodi mpya ambayo ni kolabo na msanii wa kike ambaye hakuwa tayari kumtaja, kazi ambayo itatoka rasmi mapema mwezi ujao.

Hapa unaweza kumsikiliza nyota huyu akifunguka zaidi mwenyewe;