Jumanne , 23rd Jun , 2015

Star wa michano kutoka hapa Tanzania mwenye makazi yake huko Hamburg Ujerumani, Peen Lawyer ameeleza kukua kwa muziki wa kizazi kipya kutoka Tanzania na lugha ya Kiswahili kwa ujumla, akiwa kama msanii anayefanya muziki huo kutoka nje ya nchi.

Peen Lawyer

Peenn Lawyer ameieleza eNewz kuwa, ladha hii ya muziki wa Tanzania na lugha yake imekuwa ni kitu ambacho kinapendeka sana nje, akisisitiza wasanii kuambatanisha ujumbe katika kazi zao.

Vilevile star huyo akagusia project yake mpya ya 'Mtu Flani' toleo la pili, rekodi ambayo inagusia makosa vilevile changamoto mbalimbali kurekebisha mambo yaende sawa katika jamii.