Jumatatu , 22nd Jun , 2015

Wakimbizi wa Burundi walio katika kambi ya wakimbizi Nyarugusu wilayani Kasulu mkoani Kigoma, wameiomba Jumuia ya kimataifa kuendelea kuishinikiza serikali ya Burundi kutofanya uchaguzi na kushughulikia mgogoro wa nchi hiyo mapema.

Kambi ya wakimbizi Nyarugusu

Wakimbizi wa Burundi walio katika kambi ya wakimbizi Nyarugusu wilayani Kasulu mkoani Kigoma, wameiomba Jumuia ya kimataifa kuendelea kuishinikiza serikali ya Burundi kutofanya uchaguzi na kushughulikia mgogoro wa nchi hiyo mapema ili wasiendelee kuwa wakimbizi kwa muda mrefu.

Wameeleza hayo katika kambi ya wakimbizi Nyarugusu wilayni Kasulu, ambapo wamesema bado hali ya amani ya nchi hiyo sio nzuri na ni jitihada za kimataifa pekee ndio zinaweza kuinusuru nchi hiyo kurudi katika hali yake ya kawaida.

Wamesema uchaguzi unaotarajiwa kufanyika utaongeza chuki kutokana na wananchi kuogopa na kutokuwa tayari kwa uchaguzi kutokana na kumpinga Rais Pierre Nkurunzinza kugombea tena urais wa nchio hiyo.

Kwa upande wake mkuu wa kambi ya wakimbizi Nyarugusu Sospeter Boyo, amesema kwa sasa kambi hiyo imefurika na jitihada za kuwahamishia wakimbizi wa Burundi katika eneo lililotengwa zinaelekea kukwama kutokana na eneo hilo la Migunga kutofaa kutokana na jiografia yake hali ambayo inafanya wakimbizi hao toka nchi mbili waendelee kuishi katika kambi moja .