Jumatatu , 22nd Jun , 2015

Watu wawili wamekutwa wameuawa katika mazingira ya utata mkoani Kagera Wilaya ya Misenyi katika kijiji cha Jera ambapo miili yao imekutwa na majeraha shingoni na wananchi kuhisi kuwa wametolewa makoromeo yao.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera Henry Mwaibambe.

Akiongea na East Africa Radio leo Kaimu Kamanda wa Mkoa wa Kagera Gilesi Mloto amesema kuwa tukio hilo limetokea mwishoni mwa wiki na kuongeza kuwa watu hao wameuawa katika mazingira ya uhalifu na wala si kwa kutolewa koromeo kama inavyovumishwa na wananchi.

Kamanda mloto amesema kwa mujibu wa Daktari aliyefanya uchunguzi wa miili ya watu hao amesema makoromeo yao yapo ila polisi wanaendelea na uchunguzi wa kina ila kuwabaini waliohusika na tukio hilo.

Aidha ametoa wito kwa wananchi na vyombo vya habari mkoani humo kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi pindi wanapogundua uhalifu unataka kutokea ili kutokomeza uhalifu huo ikiwemo mauaji.