Alhamisi , 20th Mar , 2014

Msanii Lameck Ditto, baada ya ukimya wa muda amerejea kwa kishindo na kazi mpya inayokwenda kwa jina Tuongeze Bidii ambayo amepanga kuiachia rasmi leo, wimbo huo unaongeza idadi ya nyimbo zake zilizo sikika katika vyombo vya habari kufikia tatu.

Kazi hii mpya ya Ditto ni kwa ajili ya kuwakumbusha mashabiki wake kuwa, mbali na ukimya wa muda mrefu yeye bado yupo katika gemu ya muziki, ingawa kwa sasa pia anatumia muda wake kushughulikia masuala ya kilimo na kutayarisha matangazo hususan ya radio.

Hapa Ditto anaongea kuhusiana na kazi yake hii.