Alhamisi , 20th Mar , 2014

Msanii wa muziki Jose Chameleone ambaye anatarajia kufunga mwezi huu kwa onyesho kubwa huko Uganda, ameweka wazi kuwa, sambamba na tukio hili, kutakuwa na uzinduzi wa video zake 7 alizozitengeneza katika ziara zake

Kwa mujibu wa taarifa, video hizi zimerekodiwa katika ziara za msanii huyu nchini Australia na Afrika Kusini, kati ya nchi nyingine ambazo ameweza kuzifikia kwa ajili ya kumwaga burudani ya muziki.

Chameleone katika onyesho lake hili litakalotoa burudani ya kumaliza mwezi, Machi 28, atapata mashavu ya kusindikizwa na wasanii wengine wakali wa Uganda, akiwepo Bobi Wine, Goodlyf, Khalifa Aganaga na wengineo.