Jumatano , 17th Jun , 2015

Chama cha Tenisi Nchini TTA kimeandaa michuano ya wazi kwa watoto na vijana itakayofanyika uwanja wa Gymkhana jijini Dar es salaam kuanzia Juni 24 mwaka huu.

Katika taarifa yake, Kocha wa Timu ya Taifa ya mchezo huo, Salum Mvita amesema, chama hicho kimeandaa mashindano hayo kwa lengo la kupata wachezaji watakaowaendeleza kwa ajili ya mashindano ya kimataifa.

Mvita amesema, wachezaji wanaotakiwa kushiriki ni kuanzia miaka tisa mpaka 24 kwa upande wa wanawake na wanaume.