Jumatatu , 15th Jun , 2015

Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa stars kinatarajiwa kuwasili nchini kesho (Jumanne) kwa ajili ya kujiandaa na michuano kuiwania kufuzu kucheza fainali za michuano ya Afrika kwa Wachezaji wanaocheza ligi za Ndani CHAN.

Stars jana ilipoteza mchezo wake wa kwanza kuwani kufuzu fainali za AFCON mwaka 2017 baada ya kufungwa na Misri bao 3-0.

Stars ilicheza vizuri kipindi cha kwanza na hasa sehemu ya ulinzi ilifanya kazi ya ziada kuokoa mashambulizi ya washambuliaji wa timu ya Misri na kupelekea kwenda mapumziko 0-0.

Kipindi cha pili Misri walifanya mabadiliko yaliyowapelekea kupata mabao hayo matatu ndani ya dakika 10.