Jumatatu , 8th Jun , 2015

20%, msanii wa muziki ambaye amekuwa kimya kwa muda mrefu sasa katika gemu ya Bongofleva, amejipanga vizuri kurejea tena akiwa amerekebisha mambo kadhaa ambayo anafikiri yameleta changamoto katika sanaa yake.

msanii wa miondoko ya bongofleva nchini 20%

Kupitia jitihada zake binafsi, 20% vilevile ameweka wazi mikakati ya kurudi upya, matumizi ya vilevi na mengine yanayofanana na hayo, huku akiwa tayari amekamilisha project inayokwenda kwa jina 'Subira' ambayo anazungumzia hapa kwa kifupi.