
Mchezaji huyo mwenye wa umri wa miaka 34, kwa sasa hana mkataba na klabu yoyote baada ya kuondoka katika klabu ya Paris St-Germain.
Ibrahimovic atakuwa ni mchezaji wa pili kununuliwa na meneja mpya wa Man United Jose Mourinho, aliyemrithi Louis van Gaal mwezi Mei.
Beki wa Ivory Coast Eric Bailly, 22, alikuwa wa kwanza kununuliwa na Manchester United kwa ada ya paundi milioni 30 kutoka klabu ya Villarreal ya Uhispania.
United pia wanaendelea kumuwinda Henrikh Mkhitaryan, raia wa Armenia anayechezea klabu ya Borussia Dortmund ya Ujerumani.
Chanzo BBC.