Jumapili , 6th Jun , 2021

Klabu ya soka ya Chelsea imesema ipo tayari kumuuza kiungo wake mshambuliaji Hakim Ziyech kwenye usajili wa dirisha kubwa msimu ujao, licha ya kukaa kwa msimu moja tu.

Hakim Ziyech akiwa na kombe la Ulaya

Ziyech anatathiminiwa kushindwa kukidhi mahitaji ya klabu ya Chelsea katika msimu huu wa kwanza huku wakiwa na matarajio makubwa kutoka kwake, hakuwa kwenye kikosi cha kwanza cha makocha wote wawili aliyofanya nao kazi Frank Lampard na Thomas Tuchel.a 

                Hakim Ziyech akikabiliana na  Trent Alexander Arnold wa liverpool

Itakumbukwa kuwa Chelsea ndiyo aliyeshinda vita vya kumnasa Ziyech kutoka klabu ya Ajax Amsterdam ya Uholanzi baada ya kuonesha kiwango kizuri kwa misimu kadhaa mfulilizo na vilabu vingi vya Ulaya kuwania saini yake vikiwemo vile vikubwa Manchester United Real Madrid, Barcelona Bayern.

Taarifa zinasema vilabu vya Italia Napoli na Ac Milan zimeweka wazi kumhitaji wa mchezaji huyu raia wa Morocco ili kuongeza nguvu kwenye vikosi vyao kwa msimu ujao na vina utayari wa kulipa dau lolote.

Takwimu za Ziyech akiwa Chelsea msimu huu wa 2020-2021 amecheza mechi 23 za EPL amefanikiwa kufunga magoli 2 na mechi 16 za mashindano mengine ikiwemo UEFA Champions League ambapo amefanikiwa kufunga magoli 4 hivyo jumla ya mabao 6 katika michezo 39.