Alhamisi , 16th Mar , 2017

Shirikisho la soka Barani Afrika (CAF) leo limepitisha ombi la Zanzibar kuwa mwanachama wake mpya bila ya kupingwa na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa shirikisho hilo uliofanyika Addis Ababa nchini Ethiopia.

Kikosi cha Zanzibar Heroes

 

Hatua hiyo inafutia maombi ya muda mrefu ya Zanzibar kutaka uanachama huo, ambapo katika mkutano mkutano wa leo imekuwa ni moja ya ajenda iliyojadiliwa na kisha kupatishwa kwa kupata theluthi mbili ya idadi ya kura  wanachama wote, maamuzi ambayo sasa yanaifanya Zanzibar kutangazwa kuwa mwanachama mpya kamili wa CAF wa 55.

Uanachama huo sasa unaifanya Zanzibar iweze kushiriki michuano ya kimataifa inayoandaliwa na CAF kama taifa kamili, ikimaamisha kuwa kuanzia sasa Tanzania (Tanzania Bara na Zanzibar) itakuwa na timu mbili katika michuano yote ya CAF ikiwemo CHAN na AFCON.

Mkutano Mkuu wa CAF ulipokuwa ukiendelea nchini Ethiopia leo

Manufaa mengine ni Zanzibar sasa kushiriki Fainali za Afrika Wanawake (Awcon), Fainali za Vijana (Afcon U-17 na U-20), kuhudhuria mikutano mbalimbali kama mwanachama kamili pia kupokea na kusimamia kozi za zitakazokuwa zinatolewa CAF.

Pia Zanzibar itakuwa na fursa ya kupiga kura katika masuala muhimu ya CAF tofauti na awali ilipokuwa inapata nafasi hiyo mpaka klabu zake ziwe zimeshika nafasi ya juu katika ligi kuu Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho.

Ahmed Ahmed

Katika hatua nyingine, shirikisho hilo leo limemchagua bwana Ahmed Ahmed kutoka Madagascar kuwa Rais wake mpya, na kumbwaga kigogo katika nafasi hiyo, Issa Hayatou ambaye ndiye aliyekuwa Rais anayemaliza muda wake.

Katika uchaguzi uliofanyika kupitia mkutano huo, Ahmed amepa kura 34 dhidi ya kura 20 alizopata Issa Hayatou.