
Kikosi cha Yanga katika moja ya mechi ya michuano ya Mapinduzi inayoendelea kushika kasi yake Visiwani Zanzibar.
Yanga ndio waliotangulia kufunga kwa Bao la Kichwa cha Amissi Tambwe katika Dakika ya 13 na URA kusawazisha Dakika ya 76 kupitia Peter Lwasa.
Katika Mikwaju ya Penati Tano Tano URA ikaibuka kidedea kwa Penati 4-3 zilizofungwa na Deo Othieno, Said Kyeyune, Jimmy Kulaba na Brian Bwete wakati za Yanga zikifungwa na Kevin Yondan, Deo Munishi na Simon Msuva huku Malimi Busungu na Geoffrey Mwashiuya wakikosa.
Kwenye Fainali URA watacheza na Mtibwa Sugar ambao mapema Jana waliwabwaga Mabingwa Watetezi wa Kombe hili Simba kwa kuwafunga 1-0.