Jumatano , 7th Nov , 2018

Klabu ya soka ya Yanga imeweka wazi sababu za baadhi ya nyota wake kutohuria mazoezi kwa kile ilichodai kuwa ni wengine kuwa na timu ya taifa na wengine kuwa majeruhi.

Wachezaji wa Yanga wakiwa mazoezini

Taarifa ya Yanga iliyotolewa leo mchana  inafuta uvumi ulionea kuwa baadhi ya wachezaji hawakuhudhuria mazoezi ya jana na leo kwasababu za maslahi.

''Kikosi kimeendelea na mazoezi yake kwenye uwanja wa Police Kurasini uku kikiwakosa wachezaji ambao wapo kwenye kambi ya timu taifa, wale wa u23 pamoja na wachezaji watatu Juma Mahadhi, Pappy Tshishimbi na Baruan Akilimali ambao bado ni majeruhi'', imeeleza taarifa hiyo.

Jana iliripotiwa kuwa baadhi ya wachezaji  wa Yanga wameshindwa kufika mazoezini hivyo kuonekana kwa wachezaji hao hii leo kumeweka sawa suala hilo.

Katika mchezo wa mwisho wa Yanga kwenye ligi kuu ililazimishwa sare ya bao 1-1 na Ndanda FC kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.