
Beki hodari wa Timu ya Azam, Pascal Wawa akiruka juu kuwania mpira na Mshambuliaji wa Timu ya Yanga, Donard Ngoma
Akizungumza hii leo Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano ya klabu ya Yanga Jerry Muro amesema wamekubali matokeo hayo kwa kuwa kwenye mchezo kuna matokeo matatu ya kushinda,kufungwa,na kutoka sare,hiyvo kutolewa kwa penati ni sehemu ya mchezo na sikwamba wachezaji wao hawajui kupiga penati.
Muro amesema kwa sasa wanajipanga na msimu mpya wa Ligi kuu ya soka Tanzania Bara ambayo inatarajiwa kuanza mwezi septemba mwaka huu.
Kwenye mchezo huo wa jana Azam ilipata penati zote tano zilizopigwa na Kipre Tchetche, John Bocco, Himid Mao, Paschal Wawa na Nahodha wa timu hiyo Agrey Morris huku kwa upande wa Yanga Salum Telela, Nahodha Nadir Canavaro,pamoja na Godfrey Mwashuiya wakitupia kambani penati zao kabla ya Haji Mwinyi kukosa Penati ya tatu iliyodakwa na kipa wa Azam Fc Aishi Salum Manula.