Wachezaji wa Yanga Malimi Busungu (katikati), Amis Tambwe (kushoto) na Haji Mwinyi (kulia) wakishangilia moja ya goli kwenye mechi za ligi kuu ya soka Tanzania bara.
Bao pekee la ushindi wa yanga lilikwamishwa kimiani na mlinzi Kevin Patrick Yondan kwa mkwaju wa penalti kipindi cha pili kufuatia kiungo Deus Kaseke kuangushwa na Hemed Khoja aliyemkwatua kwa nyuma kwenye eneo la hatari.
Jabla ya bao hilo yanga ilikosa penati iliyopigwa na Amis Tambwe dakika ya 47 iliyopatikana baada ya beki wa Ndanda, Paul Ngalema kumuangusha winga Simon Msuva kwenye boksi.
Kwa matokeo hayo Yanga sasa wanakaa kileleni mwa ligi kuu kwa wastani wa mabao tu, wakiwa wamefunga mabao 31 na kufungwa matano, wakati Azam FC imefunga mabao 28 na kufungwa tisa.
Matokeo mengine ya wikiend iliyopita
Azam FC 1 African Sports 1
Simba SC 1-0 Mtibwa Sugar
JKT Ruvu 1-5 Mgambo JKT
Toto Africans 0-1 Prisons
Stand United 1-0 Kagera Sugar
Mbeya City 1-0 Mwadui FC
Coastal Union 1-1 Majimaji