.jpg?itok=W1SedMeM×tamp=1595839667)
Aliyekuwa kocha wa Yannga Luc Eymael akiongea na waandishi wa Habari.
Taarifa iliyotolewa na Klabu ya Yanga ya kumfuta kazi kocha Luc Eymael, imesema uongozi wa klabu hiyo umesikitishwa na kauli zisizo za kiungwana na za kibaguzi zilizotolewa na kocha huyo na kusambaa katika mitandao ya kijamii na vyombo mbali mbali vya habari.
Hivyo kutokana na kauli hizo zisizo za kiungwana nakiuanamichezo, uongozi wa Yanga umeamua kumfuta kazi kocha Luc Eymael kuanzia leo tarehe 27 julai na kuhakikisha anaondoka nchini haraka iwezekanavyo.
Lakini pia taarifa hiyo ya Yanga iliyotolewa na kaimu katibu mkuu Wakili Simoni Patrick umeomba radhi Viongozi wanchi, Shirikisho la mpira wa miguu Tanznaia TFF, Wanachama, Wapenzi na Mashabiki wa Yanga pamoja na wananchi kwa ujumla kutokana na kauli za kuudhi zilizotolewa na kocah Luc Eymael.
Kocha Luc alijuinga na klabu ya Yanga mwezi January akichukua nafasi ya Charles Boniface Mkwasa ambaye alikuwa kocha wa muda baada ya kocha Mwinyi Zahera kufukuzwa kazi.
Mbeligiji huyo amekiongoza kikosi cha Yanga kumaliza katika nafasi ya pili kwenye Ligi kuu Tanzania bara msimu wa 2019-20 uliomalizika jana.