Jumanne , 11th Jul , 2017

Klabu bingwa ya Ligi kuu Tanzania Bara Yanga imeanza kuwafua wachezaji wake kwa mazoezi madogo madogo kwa ajili ya kujiandaa na msimu ujao wa ligi kuu na mashindano ya kimataifa kwenye uwanja wa uhuru Jijini Dar es Salaam.

Wachezaji wa Yanga wakifanya mazoezi yao leo katika uwanja wa Uhuru Jijini Dsm.

Katika mazoezi hayo Kocha Mkuu mwenye uraia wa Zambia, George Lwandamina ameonekana kukinoa kikosi hicho kipya kikiwa na wachezaji wapya kama Ibrahim Ajibu na Abdallah Haji Shaibu 'Ninja'.

Katika hatua nyingine, Yanga imesajili mlinda mlango mpya Youthe Rostand  raia wa Cameroon miaka miwili akitokea klabu ya African Lyon hivi karibuni ili aweze kusaidiana na Beno Kakolanya baada ya zile tetesi zikidai Ally Mustafa kuondoka kwenye kikosi hicho cha Jangwani na amekuwa akihusishwa kujiunga na Singida United.