Nyota wa Yanga Fiston Mayele na Feisal Salum wakishagilia.
Akizungumza na waandishi wa habari Manara amesema kuwa wanatambua mchezo huo utakuwa mgumu lakini wanaamini kwamba watapata ushindi kwenye mchezo huo.
“Tunatambua kwamba mchezo wetu utakuwa mgumu lakini tupo tayari kwa ajili ya kusaka ushindi na tuna amini kwamba nawezekana mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi,” amesema Haji Manara .
Yanga inaongoza ligi ikiwa na pointi 48 baada ya kucheza mechi 18 inatarajiwa kukutana na Azam FC Aprili 6, Uwanja wa Azam Complex.



