Jumapili , 19th Sep , 2021

Moja kati ya Vilabu Vinne vinavyo iwakilisha Tanzania kimataifa, Klabu ya Yanga leo imeondolewa rasmi kwenye michuano ya klabu Bingwa Africa katika hatua ya awali baada ya kupoteza tena na mchezo wa mkondo wa pili uliopigwa kwenye Dimba la Adokiye Port Harcourt Nchini Nigeria kwa kufungwa

Wachezaji wa Yanga SC na Rivers United wakigombea mpira

Ikumbukwe Yanga waliingia kwenye mchezo huu wakiwa na kumbukumbu ya kufungwa pia goli moja kwa sifuri katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa wiki iliyopita katika Dimba la mkapa jijini Dar es salaam.

Mapema kabla ya chezo huu Yanga walitoa malalamiko yao kuhusu kufanyiwa hujuma ya kupewa chumba kidogo cha wachezaji kubadilishia nguo kisicho kidhi haja, kitendo ambacho kilisababisha wachezaji kubadilishia nguo uwanjani katika eneo la kukaa wachezaji wa akiba na benchi la ufundi.

Vile vile wawakilishi hao wa Tanzania walilalamikia kucheleweshwa kwa matokeo ya vipimo vya Covid- 19 ambavyo vililetwa takribani dakika 45 kabla ya mchezo kuanza na kuonyesha kwamba baadhi ya wachezaji wa yanga walio kwenye kikosi cha kwanza wana maambukizi ya virusi vya Corona wakiwemo mlinda mlango Djidgui Diarra, Viungo Mukoko Tonombe, Fisal Salum na Mshambuliaji Yacouba Sogne.

Uongozi wa klabu ya yanga ulionesha kutokubaliana na kugomea Matokeo yan vipimo hivyo, na baadae wachezaji hao walijumuishwa kwenye kikosi kilicho cheza mchezo huo. Hivyo Yanga wanatarajiwa kuanza safari ya kurudi nchini usiku wa leo baada tu ya mchezo huo kumalizika.