Wachezaji wa Yanga SC wakishangilia goli
Mchezo huo uliopigwa kwenye uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga, ulikuwa na mvutano wa aina yake kwa timu zote kushambuliana huku Prison wakitangulia kwa goli la dakika ya 51 lililofungwa na Jumanne Elifadhili.
Yanga waliendelea kushambulia kwa kasi na mashambulizi yao yakazaa matunda dakika ya 76 kwa kupata goli la kusawazisha kupitia kwa Saidi Ntibazonkiza.
Katika michezo mingine iliyopigwa leo klabu ya Klabu ya Azam FC imepata ushindi wa goli 1-0 ugenini dhidi ya Polisi Tanzania. Goli la Azam FC limefungwa na Ismail Aziz dakika ya 88.
Wachezaji wa Azam FC wakishangilia goli
Jijini Tanga klabu ya Namungo FC imepata sare ugenini dhidi ya wenyeji Coastal Union.