Jumapili , 19th Apr , 2015

Pamoja na wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya vilabu barani Afrika timu ya Dar es Salaam Yanga Afrikans kubanwa mbavu nyumbani na timu ya Etoile du Sahel ya Tunisia mashabiki na wanachama wa klabu hiyo hawajakata tamaa ya kusonga mbele

Kiungo mshambuliaji wa Yanga Simon Msuva akiangushwa na kipa wa Etoile du Sahel na kuipatia Yanga penati iliyowapa goli pekee

Wanachama na mashabiki wa klabu ya soka ya Yanga wametakiwa kuwa watulivu katika kipindi hiki ambacho wawakilishi hao wa Tanzania katika michuano ya kimataifa wakijipanga kuelekea mchezo wa marudiano dhidi ya Etoil Du Sahel ya Tunisia utakaopigwa wiki mbili zijazo huko Tunisia

Wakiongea na muhtasari wa michezo hii leo baadhi ya wanachama hao toka tawi la umoja Tandale kwa mtogole jijini Dar es Salaam Juma Miraji na Kharid Mumin wamesema matokeo ya sare ya bao 1-1 si mabaya na hivyo wanautaka uongozi na benchi la ufundi kujipanga na mchezo wa marudiano na wanaimami kubwa na timu yao kuweza kufanya maajabu katika mchezo huo ambao utakua mgumu mno

Aidha wanachama hao wamesema hakuna muda wa kupoteza kutafuta mchawi cha msingi ni viongozi na benchi la ufundi kuweka mbele mipango na mikakati mizito yakiufundi yakuhakikisha timu hiyo inajipanga nakufanya maandalizi mazito ya kuhakikisha timu hiyo inapata matokeo yatakayoiwezesha kusonga mbele kwa hatua inayofuata

Wakimalizia wnachama hao wamesema dawa ya kupata matokeo mbele ya timu hiyo ya Tunisia ambayo ni moja ya timu bora barani Afrika ni mandalizi makini yakichagizwa na ushirikiano wa wadau na wanachama na timu yote kwa ujumla wakiwemo viongozi.

Baada ya matokeo hayo ya sare ya bao 1-1 sasa yanga ili ivuke kikwazo hicho itahitaji sare ya kuanzia mabao 2-2 au zaidi au ushindi wa aina yoyote na hivyo kucheza mchezo wa mwisho wa mchujo na moja ya timu ambazo zitashindwa toka klabu bingwa barani afrika hatua ya 16 na kama ikishinda na mchujo huo ndio watatinga hatua ya robo fainali au nane bora ya kombe la shirikisho barani afrika CAF.