Yanga kuwakosa Ngoma, Tabwe na Niyonzima

Thursday , 16th Feb , 2017

Klabu ya Yanga Jumamosi hii katika mechi ya marudiano dhidi ya klabu ya Ngaya De Mbee ya Comoro itawakosa wachezaji wake watatu kutokana na wachezaji hao kuwa majeruhi

Akiongea na waandishi wa habari Kocha msaidizi wa klabu hiyo Juma Mwambusi amesema wachezaji hao ni pamoja na Donald Ngoma, Amis Tabwe pamoja na Haruna Nyiyonzima

"Tunajivunia ushindi mnono tulioupata ugenini kwani ni hazina tosha kwetu lakini tunatambua umuhimu wa mchezo wetu wa marudiano ambao utafanyika siku ya Jumamosi kwenye uwanja wa Taifa, kikubwa nawaomba mashabiki wetu na wanamichezo wajitokeze kwa wingi kuipa sapoti timu yao. Lakini katika kuelekea mchezo huo wachezaji tutakao wakosa sababu ya majerui ni Ngoma, Tambwe na Haruna" alisema Juma Mwambusi

Mbali na hilo viingilio kuingia mechi hiyo siku ya Jumamosi vimetangazwa katika viti vya Mzunguko kiingilio itakuwa Tsh 3000, VIP A - Tsh 20,000, VIP B -Tsh 10,000, VIP C -Tsh 10,000.