Jumamosi , 6th Aug , 2016

Yanga inashuka dimba la Taifa jijini Dar es salaam leo kukipiga na Mtibwa Sugar katika mchezo wa kirafiki huku ikitarajiwa kuwakosa nyota wake watatu.

Mawinga wa Yanga, Simon Msuva (kulia) na Geoffrey Mwashiuya (kushoto)

Nyota hao Juma Abdul anasumbuliwa na Malaria na mawinga Geoffrey Mwashiuya na Simon Msuva wanasumbuliwa na maumivu ya goti.

Mchezo huo utafanyika baada ya kumalizika kwa Mkutano Mkuu wa dharula wa klabu hiyo unaofanyika kuanzia asubuhi ya leo.