Jumatatu , 12th Nov , 2018

Klabu ya soka ya Yanga imetangaza mechi yake nyingine ya kirafiki ikiwa ni sehemu ya mipango yake ya kujiandaa na mchezo wa ligi kuu soka Tanzania bara dhidi ya Mwadui Fc Novemba 22, 2018.

Wachezaji wa Yanga wakiwa benchi kwenye moja ya michezo ya timu hiyo.

Baada ya jana kucheza na African Lyon na kushinda bao 1-0, Yanga imeweka wazi kuwa itacheza na Reha FC ambayo inashiriki ligi kuu soka daraja la kwanza.

Mchezo huo utapigwa Jumatano, Novemba 14, 2018, kwenye uwanja wa uhuru jijini Dar es salaam. Viingilio ambavyo vimetajwa ni 5000 kwa jukwaa kuu na 3000 mzunguko.

Hivi karibuni Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Omary Kaya aliweka wazi kuwa timu hiyo inakusudia kucheza michezo mitatu ya kirafiki kabla ya kwenda mkoani Shinyanga kwaajili ya mchezo na Mwadui Fc.

Yanga ipo katika nafasi ya 3 kwenye msimamo wa ligi, ikiwa na alama 26 kwenye michezo 10 iliyocheza mpaka sasa.