Jumanne , 4th Apr , 2017

Uongozi wa mabingwa watetezi wa ligi kuu ya soka Tanzania bara Yanga katika vita ya kutetea ubingwa wao wa ligi, ubingwa wa Kombe la Shirikisho na pia kujipanga na mchezo wa kombe la shirikisho siku Jumamosi dhidi ya MC Algiers ya Algeria.

Kikosi cha Yanga

Kutokana na vita hizo za aina tatu tofauti, uongozi huo umewataka wanachama wa klabu hiyo kuwa watulivu katika kipindi hiki muhimu na kinachohitaji tahadhari kubwa.

Katibu mkuu wa Yanga Charles Boniface Mkwasa amesema hayo wakati akizungumza na Kipenga ya EA Radio juu ya mipango yao mkakati baada ya kukalia usukani wa ligi kuu kuelekea michezo mitano iliyosalia sambamba na ule wa kimataifa dhidi ya Waalgeria.

Mkwasa amesema ingawa kwa sasa wanaongoza ligi, lakini ni vigumu sana kuendelea kukaa katika nafasi hiyo hivyo wanahitaji umakini wa hali ya juu katika michezo iliyobaki na hatimaye kumaliza ligi wakiwa mabingwa.

Msikilize hapa Mkwasa