Jumanne , 26th Jul , 2022

Waziri wa Habari na Teknolojia Nape Nnauye anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika pambano la Pay Back Night Songea linalotarajia kupigwa Julai 30, mwaka huu kwenye Uwanja wa Majimaji uliopo mjini hapa.

Waziri wa Habari na Teknolojia Nape Nnauye

katika pambano hilo ambalo Mtanzania, Seleman Kidunda atapanda ulingoni kuwania mkanda wa ubingwa wa Dunia wa WBF dhidi ya  Tshimanga Katompa kutoka DR Congo.

Promota wa pambano hilo kutoka Peak Time Media, Meja Seleman Semunyu ameweka wazi kwa kusema kuwa tayari wameshapata baraka za mkoa kutoka kwa mkuu wa mko wa Ruvuma, Brigedia Jenerali, Balozi Wilbert Ibuge kuelekea kwa pambano hilo ambalo mgeni wake rasmi wanatarajia kuwa ni Waziri wa Habari na Teknoloaji, Nape Nnauye.

“Pambano hili limepata baraka za kimkoa, niwaambie sasa Watanzania na wadau wa masumbwi kwamba tupo tayari kwa ajili ya pambano hapa, ulingo umeshafika na niwaambie mgeni rasmi siku ya pambano atakuwa ni waziri Nape Nnauye,” amesema  Semunyu.

 Lakini kwa upande wa mkoa wa mkoa, Brigedia Jenerali, Balozi, Wilbert Ibuge alisema kuwa ni heshima kubwa kwa bondia huyo kwa kuwa jeshi la wananchi halijawahi kushindwa huku akiwatakia heri mabondia wote watakaopanda ulingoni siku hiyo pamoja na kuwaomba wakazi wa mkoani hapa kujitokeza kwa wingi siku hiyo.

Hata hivyo Kidunda alipata nafasi ya kukutana na Brigedia Jenarali CP Feruzi ambaye  kamanda wa brigedi  Kanda ya Kusini wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania alisema kuwa ni heshima kubwa kwa mchezo huo kupelekwa mkoa humo kwa kuwa ana zaidi ya miaka minne hajawahi kushuhdia mchezo ukifanya mkoani hapa ambapo amewatakia ushindi mabondia wote  wakiwemo wa jeshi watakaopanda ulingoni kwenye pambano hilo.