Jumatano , 26th Nov , 2014

Wazazi nchini wametakiwa kuwapa watoto nafasi ya kushiriki na kujifunza michezo mbalimbali ili kuweza kukuza uwezo wao wa kufikiria na kukuza vipaji vyao.

Akizungumza na East Africa Radio,Mkamu wa Rais wa Chama cha mchezo wa Gofu nchini,Joseph Tango amesema wameanzisha programu ya kukuza vipaji vya michezo kwa watoto lakini kumekuwa na changamoto nyingi kwa upande wa wazazi ambao imekuwa vigumu kuwaruhusu watoto hao kupata nafasi ya kujifunza.

Tango amesema hivi sasa wanaendelea na programu hiyo katika viwanja mbalimbali ambapo wamepata baadhi ya wanafunzi ambao wanauelewa kuhusu michezo hususani mchezo wa Gofu ambao unaanza kukua hapa nchini.