
Mtendaji Mkuu na Afisa Habari wa klabu ya Simba.
Hayo yameelezwa na Mtendaji wa klabu, Crescencius Magori katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es salaam wakati wa kutangaza maamuzi kadhaa ya Bodi ya Wakurugenzi wa klabu hiyo.
Magori amesema kuwa Bodi ya muda ya Klabu ya Simba ( Interim Board) ilimteua Kaimu Mtendaji Mkuu wa Klabu kwa kipindi cha Miezi 6, hivyo sasa Bodi imeridhia matakwa yake ya kutoendelea na kazi hiyo na imemuomba kwa kipindi cha miezi miwili( siku 60) aendelee ili Bodi pamoja na yeye mwenyewe wasimamie upatikanaji wa Mtendaji Mkuu mpya pamoja na Waajiriwa wengine.
Hivyo nafasi ya Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simba pamoja na Wakurugenzi zitatangazwa kwa Watanzania na wasio Watanzania hivi karibuni na kusisitiza kuwa watu wenye uwezo na vigezo vya kufanya kazi na Kampuni ya Simba kutosita kuleta maombi punde kazi zitakapotangazwa.
Aidha Magori amesema maandalizi ya Simba day yatafanyika kama kawaida na katika kilele cha siku hiyo, Simba itazindua wimbo mpya wa klabu hiyo chini ya mratibu wa kazi hiyo, Haji Manara.
Aidha kuhusiana na sakata la hati za klabu hiyo lililoibuliwa na Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini, Mzee Hamis Kilomoni, Mtendaji Magori amesema, "hiyo hati iliyoshikiliwa haiwezi kuzuia mabadiliko ndani ya Simba. Hawa wazee siyo walioianzisha Simba, walioianzisha walishakufa, na wao watakufa, na hata sisi tutakufa, watakuja wengine”, amesema.