Alhamisi , 1st Oct , 2015

Wachezaji wanne wa Timu ya taifa ya Gofu ya Tanzania wameondoka leo nchini kuelekea mombasa nchini kenya kwa mashindano ya Kimataifa ya kirafiki yatakayofanyika kwa siku 2 wikiend hii.

Wachezaji wanne wa Timu ya taifa ya Golf ya Tanzania wameondoka leo nchini kuelekea mombasa nchini kenya kwa mashindano ya Kimataifa ya kirafiki yatakayofanyika kwa siku 2 wikiend hii.

Akizungumza jijini Dar es Salaam hii leo, Rais wa chama cha gofu Tanzani, TGU Joseph Tango amesema ushiriki wa timu hiyo katika mashindano hayo yatakayoshirikisha nchi za Kenya na Uganda yataimarisha wachezaji wa Tanzania wanaojiwinda na michuano ya Afrika .

Ameongeza kuwa mara baada ya wachezaji hao kurejea nchini wataweka kambi jijini Arusha kwa ajili ya maandalizi michuano ya East Africa Challenge itakayofanyika Novemba 16 hadi 22 mwaka huu.

Tango amewaomba watanzania wajitokeze kujifunza mchezo wa gofu hasa vijana kuanzia umri wa miaka 6 hadi18 ili kupata timu itakayoshiriki mashindano mbalimbali ya kimataifa kwa baadaye.