Jumapili , 17th Mei , 2015

Kamati ya Olimpiki nchini TOC imewataka vijana watatu wanariadha waliochaguliwa kujiunga na kambi iliyo Eldoret nchini Kenya kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya Olimpiki kufuata sheria za michezo.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Rais wa TOC, Gulam Rashid amesema, vijana hao wanatakiwa kufuata maadili ya kituo kwa kufuata mambo muhimu waliyopangiwa ili kuweza kuwa na maendeleo mazuri katika maandalizi hayo.

Gulama amesema, kambi hiyo inatarajiwa kuanza kesho ambapo wanamichezo hao wanaakiwa kufuata mambo ambayo yatachangia kuendeleza mkataba wao ikiwemo kuachana kabisa na madawa ya kuongeza nguvu katika michezo.