Kocha wa zamani wa Simba Dylan Kerr kabla ya kutimuliwa klabuni hapo jana
Wakizungumza na East Africa Radio wanachama hao wakiwa katika maskani ya klabu hiyo mitaa ya Msimbazi wamesema wanaunga mkono uamuzi huo japo umechelewa lakini pia wanautaka uongozi nao ujitathmini kwa namna wanavyoiendesha klabu hiyo.
Hassan Salum ambaye ni mwanachama kutoka tawi la wekundu wa Terminal amesema timu yao ilikuwa ikicheza kwa kiwango cha chini licha ya kupata matokeo mazuri jambo ambalo lingewagharimu kwenye mashindano ya kimataifa endapo wangetwaa ubingwa wa ligi kuu au wa kombe la shirikisho.
Naye katibu msaidizi wa tawi la Temeke Koma Mohamed Hassan amewaasa viongozi wa klabu hiyo nao kujitathmini kwa kina na endapo baadhi yao hawatoshi kuiongoza klabu ni vyema nao wakawajibishwa kama ilivyo kwa makocha.


