Wanamichezo vijana wa Tanzania chini ya miaka 15 wakiwa katika michuano ya vijana ya Africa huko Botswana.
Serikali imepokea bendera ya taifa kutoka kwa wachezaji wa timu ya Tanzania iliyoshiriki michuano ya Olimpiki ya Afrika kwa vijana chini ya miaka 15,michuano iliyofanyika nchini Botswana na kuhitimishwa mwishoni mwa mwezi mei,mwaka huu
Akizungumza jijini Dar es salaam,wakati wa hafla ya kuwapongeza vijana hao, Mkurugenzi wa maendeleo ya Michezo Leonard Thadeo amesema wadau mbalimbali wenye uwezo wajitokeze kuanzisha timu mbalimbali za vijana za michezo tofauti kwani vipaji huanzia chini
Thadeo amewataka vijana hao kuwa na nidhamu na kujitunza kwa kufuata taratib za kimichezo kama wanataka kuendelea mbele na kutunza vipaji vyao
Naye rais wa kamati ya Olimpiki Tanzania TOC Ghuram Rashid pamoja na pongezi kwa vijana hao pia ametoa wito kwa vyama vyote kujipanga na kuhakikisha wanakua na timu bora ambazo zitashiriki michuano yote katika msimu mwingine wa mwaka 2018
Kwaupande wake nahodha wa timu hiyo ambayo ilikua na wachezaji wa riadha, kuogelea na na mpira wa miguu amabo walifanikiwa kutwaa medali ya fedha Thomas Chindeka ametoa shukrani kkwa wadau wote waliofanikisha maandalizi ya timu yao na kuwaunga mkono mpaka hapo walipofikia.