Jumatatu , 3rd Nov , 2014

Wakufunzi wa mpira wa miguu wanawake waliomaliza muda wao hapa nchini wametakiwa kujitokeza kwa ajili ya kuwafundisha wakufunzi wanawake katika ngazi za awali ili kuweza kupata waamuzi wa soka la wanawake hapa nchini.

Akizungumza na East Africa Radio, Mmoja wa wakufunzi wa waamuzi wa Shirikisho la Soka Ulimwenguni FIFA, Sudi Abdi amesema mafunzo waliyoyapata katika kozi hiyo yamewasaidia ambapo kulikuwa na baadhi ya wanawake waliokuwa wakionesha nia katika mafunzo hayo.

Abdi amesema iwapo wanawake watajitokeza kwa wingi kwa ajili ya kufundisha soka, itasaidia kwa kiasi kikubwa kukuza timu za wanawake nchini na pia kuondokana na suala la kuwa na makocha wa kigeni kwa ajili ya kufundisha timu mbalimbali za wanawake.