Alhamisi , 12th Oct , 2023

Wajumbe 89 kutoka chama cha mpira wa miguu Temeke (TEFA) wamepinga mchakato mzima wa uchaguzi mkuu kutokana na kutorodhishwa na mwenendo wa kutofuatwa kwa katiba ya chama hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari Leo Oktoba 12, 2023 Katibu wa klabu na wanachama Habibu Hamadi amesema kwa umoja wao hawapo tayari kushiriki uchaguzi huo kutokana na baadhi ya katiba kuvunjwa ili wawapitishe wagombea wao.

“Uchaguzi wa TEFA ulikuwa ni kujaza nafasi ya Mwenyekiti iliyoachwa wazi baada ya aliyekuwa Mwenyekiti kufariki dunia, hiyo ndio ilikuwa dhima ya uchaguzi wa TEFA.

Wanachama wa Mkutano Mkuu wa TEA wakafanva Mkutano wa kikatiba na kuridhia kwamba, Makamu Mwenyekiti wa kwanza akaimu nafasi ya Mwenyekiti aliyefariki na Makamu wa pili akaimu nafasi ya Makamu wa kwanza halafu wasubiri uchaguzi mkuu mwezi Machi mwakani”amesema  Hamadi.

Nao wajumbe wa TEFA wameiomba  Wizara ya Utamaduni ,Sanaa na Michezo chini ya Waziri wake Dokta Damasi Ndumbaro  pamoja na Baraza la Michezo kuingia katika swala hilo kwa maendeleo ya michezo katika wilaya ya Temeke.

Uchaguzi wa TEFA ulikuwa ni kujaza nafasi ya Mwenyekiti iliyoachwa wazi baada ya aliyekuwa Mwenyekiti kufariki dunia, hiyo ndio ilikuwa dhima ya uchaguzi wa TEFA.