Jumatatu , 20th Jun , 2016

Klabu ya Tottenham Hotspur imekubali kumsajili kiungo wa kati wa Southampton mkenya Victor Wanyama kwa kima cha pauni milioni 11.

Inaaminika kuwa wanyama mwenye umri wa miaka 24, ambaye alijiunga na Southampton akitokea Celtic mwezi Julai mwaka 2013 kwa pauni milioni 12.5, kwa sasa anafanyiwa uchunguzi wa kiafya.

Wanyama atakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na klabu hiyo na ataungana na meneja wake wa zamani Maurico Pochettino.

Chanzo BBC