
Victor Costa 'nyumba'
Costa amefunguka hayo katika mkutano wa kampeni ya uchaguzi mkuu ujao ndani ya klabu hiyo uliofanyika eneo la Kata 14, Temeke jijini Dar es salaam ambapo yeye alikuja kumsapoti mkewe, Jasmine Badar ambaye ni mmoja ya wagombea.
"Suala la kugombea hilo lipo, kwa siku za usoni ndio malengo yangu makubwa kwasababu katika michakato tunayokwenda nayo unaona kabisa ni michakato ya maendeleo, kwahiyo na mimi hayo ndio malengo yangu", amesema Costa.
Aidha, mkewe ambaye ni mgombea katika uchaguzi huo, katika kampeni yake amesema kuwa ameamua kugombea tena ili ayaendeleze yale aliyoyaanzisha katika klabu hiyo hasa katika soka la wanawake.
"Nimehakikisha timu ya wanawake imecheza mpaka ikaingia hatua ya nane bora ikiwa haina bajeti ya klabu, lakini kama mwanamke nimepambana kwenye bodi", amesema Jasmine, akijininadi katika mkutano huo wa kampeni.
Kampeni za uchaguzi mkuu wa kuchagua viongozi mbalimbali wa klabu ya Simba zinatarajia kuhitimishwa, Novemba 3 kabla ya tarehe ya uchaguzi huo ambayo ni Novemba 4 mwaka huu.