Ijumaa , 1st Jan , 2016

Kocha wa Manchester United Luis Van Gaal amesema hakuna miujiza kwa timu hiyo kurejesha bahati endapo jitihada hazitofanyika.

Kocha wa Manchester United Luis Van Gaal amesema hakuna miujiza kwa timu hiyo kurejesha bahati endapo jitihada hazitofanyika.

Akizungumza kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Swansea City,Van Gaal amesema mambo hayatobadilika bila ya kutambua makosa na kujirekebisha kwa timu nzima na mchezaji mmoja mmoja.

Van Gaal,ambaye kikosi chake hakijashinda mechi 8 zilizopita hadi sasa amesema amejipamga vyema kuhakikisha wanashinda mchezo wa kesho dhidi ya Swansea City,kwa kuwa katika mechi tatu alizokutana na timu hiyo amepoteza zote.